Hirisi

Je Mungu asemaje kuhusu hirizi? Imo katika Biblia, Isaya 2:6 "Maana wewe umewaacha watu wako, nyumba ya Israeli kwa sababu wamejaa kawaida za mashariki nao niwapiga ramli kama wafilisti na wanapana mikono na wana wa wageni." Isaya 3:18-20 "Siku hiyo Bwana atawaondolea uzuri wa njunga zao na kaya zao; na pete za masikio na vikuku na taji zao; na dusumali na mafurungu na vitambi na vibweta vya marashi na matalasimu."

Hirizi ilikuwa jambo la kawaida wakati wa zama za wayahudi, hususan kati ya wapagani. Hirizi ilitumiwa kuwalinda watu kutokana na mashetani, magonjwa na ajali na pia kuleta bahati njema. Hirizi hizi zipo katika mifumo ya kioo zina valiwa katika viunoni kama bangili, pete, shanga na mikufu shingoni. Hirisi hizi zilijulikana na kwamba zina nguvu Fulani zinazo kinga mtu kutokana na maasi na kuleta utajiri. Pia zina leta nguvu za kuponya.

Wakati wa wana Waisraeli walichukua desturi na mila za watu wasiomjua Mungu pamoja na hirizi, Mungu alitoa amri kali kuhusu uvaaji wa hirizi. Imo katika Biblia, Ezekieli 13:18, 20, 21 "Useme Bwana Mungu wangu asema hivi; ole wao wanawake wale washonao hirizi katika viungo vyao vya mikono wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo ili wawinde roho za watu je mtazishinda roho za watu wangu? na kuzihifadhi roho zenu wenyewe? Basi Bwana MUNGU asema hivi; tazama mimi ni kinyume cha hirizi zenu ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu nami nitazishikilia roho zile mnazoziwinda kama ndege na leso zenu nazo nitazirarua na kuwaokoa watu wangu katika mikono yenu wala hawatakuwa katika mikono yenu tena kuwindwa; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA."

Wapagani walikuwa na vitu vilivyoitwa "terafim" mfano wa miungu waliyo iweka katika nyumba zao na kwenda nazo wanapo safiri. Mungu aliwaonya watu kuhusu tabia hizi. Imo katika Biblia, 2Wafalme 23:24 "Tena wenye pepo wa utambuzi na wachawi na vinyago na sanamu na machukizo yote yaliyoonekana katika nchi ya Yuda na katika Yerusalemu Yosia akayaondoa yote ili apate kuyadhibitisha maneno ya torati yaliyoandikwa katika kile kitabu alichokiona Hilkia kuhani ndani ya nyumba ya BWANA."

Zaburi 31:6 yasema "Na wachukia wao washikao yasiyofaa yenye uongo bali mimi na mtumaini BWANA."