Home / Masomo ya Biblia / Kusamehe

Kusamehe

Mungu yuko tayari na anasubiri kumsamehe mtu anaye omba msamaha imeandikwa Zaburi 86:5 "Kama wewe Bwana u mwema, umekuwa tayari kusamehe, na mwingi wa fadhili kwa watu wote wakuitao".

Daudi aliweka wapi tumaini yake ya msamaha? imeandikwa Zaburi 51:1 "Ee Mungu unirehemu sawasawa na fadhili zako kiasi cha wingi wa rehema zako uyakute makosa yangu."

Rehema ya Mungu I kiasi gani? Imeandikwa Zaburi 103:11-12 "Maana mbingu zilivyo inuka juu ya nchi kadiri ili ile rehema zake ni kuu kwa wamchao kama mashariki ilivyo mbali na magaribi, nidvyo alivyoweka dhambi zatu mbali nasi."

Wanao omba wasamehewe wana ahadi gani? imeandikwa 1john 1:9 "Tukiziungama dhambi zetu, yeye nimwaminifu na wahaki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote."
Naweza kusamehewa nikiwa nina kisasi na mtu mwingine? Imeandikwa Mathayo 6:14-15 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao na Baba wenu wa mbinguni atawasamehe ninyi bali msipowasamehe watu makosa yao wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu."

Wale wamesamehewa husamehe. imeandikwa Waefeso 4:32 "Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma ninyi mkasameheane kama na Mungu katika kristo alivyowasamehe ninyi."
Kusamehe kwa kweli hahesabu makosa. imeandikwa Mathayo 18:21-22 "Kisha petero akamwendea akamwambia Bwana ndugu yangu anikose mara ngapi nami ni msamehe? hata mara saba? Yesu akamwambia sikwambii mara saba bali hata saba mara sabini."

Tunapo samehewa je? ni lazima tuwena hofu? Imeandikwa Zaburi 32:5 "Nalikujulisha dhambi yangu, wala sikuuficha upotovu wangu Nalisema nitakiri maasi yangu kwa Bwana nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu."

Katika kusamehe Yesu ametukomboa kutoka kwa dhambi na mshahara wa dhambi. Imeandikwa Wakolosai 2:13-14 "Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu aliwafanya hai pamoja naye akisha kutusamehe makosa yote akisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake iliyo kuwa na uwadui kwetu akiondoa isiwepo tena akaigongomea msalabani."

Tunapo hitaji msamaha tufanye nini? imeandikwa Zaburi 51:2-4 "Unioshe kabisa na uovu wangu, unitakase dhambi zangu. maana nimejua makosa yangu na dhambi yangu I mbele yangu daima Nimekutenda dhambi wewe peke yako na kufanya maovu mbele za macho yako. wewe ujulikane kuwa unahaki unenapo, na kuwa safi utopo hukumu."

Jambo la pili omba msamaha wa dhambi zako imeanidikwa Zaburi 51:7-12 "Unisamehe kwa ihopo nami nitakuwa safi, unioshe nami nitakuwa mweupe kuliko dheluji unifanye kusikia furaha na shangwe, mifupa ilio ponda ifurahi. usitiri uso wako usitazame dhambi zangu uzifute hatia zangu zote Ee Mungu uniumbie moyo safi uifanye upya roho iliyo tulia ndani yangu usinitenge na uso wako wala roho wako mtakatifu usiniondolee unirudishie furaha ya wakovu wako unitegemeze kwa roho ya wepesi."

Jambo la tatu kuwa na imani kuwa Mungu amekusamehe na dhambi zako imeandikwa Zaburi 32:1-6 "Heri aliyesamehewa dhambi na kusitiriwa makosa yake heri Bwana asiyemhesabia upotovu, ambaye rohoni mwake hamna hila niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa kwa kuugua kwangu mchana kutwa na kwa maana mchana na usiku mkono wako ulinilemea jasho langu likakauka hata nikawa kama nchi kavu wakati wa kaskazi nalikujulisha dhambi yangu wala sikuuficha upotovu wangu nalisema nitayari maasi yangu kwa Bwana naweukanisamehe uoptovu wa dhambi yangu kwa hiyo kila mtu mtauwa akuombe wakati unapopatikana hakika maji makuu yafurikapo hayatamfikia yeye."