Home / Masomo ya Biblia / Kutunza sabato

Kutunza sabato

Ni kwa umuhimu gain tutunze sabato? Imeandikwa, Kutoka 20:8 "Ikumbuke siku ya sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote, lakini siku ya saba ni sabato ya Bwana Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi na bahari na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya sabato akaitakasa."

Sabato yaanaza wakati upi? Imeandikwa, Mambo ya walawi 23:32 "Itakuwa kwenu sabato ya kustarehe kabisa, nanyi mtazitesa nafsi zenu; siku ya kenda ya mwezi wakati wa jioni tangu jioni hata jioni mtaishika hiyo sabatu yenu."

Jioni yaazna wakati gani? Imeandikwa, Marko 1:32 "Hata kulipokuwa jioni na jua limekwisha kuchwa walikuwa wakimleteaa wote waliokuwa hawawezi na wenye pepo."

Kazi isifanywe siku ya sabato. Imeandikwa, Kutoka 20:9-10 "Siku sita utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni sabato ya Bwana Mungu wako; Siku hiyo usifanye kazi yo yote wewe wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala nyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya alango yako."

Isaya asema nini kuhusu utunzaji wa sabato?. Imeandikwa, Isaya 58:13-14 "Kamakugeuza mguu wako usihalifu sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu, ukiita sabato siku ya furaha na siku takatifu ya Bwana yenye heshima ukiitukuza kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe wala kuyatafuta ya kupendezayo wala kusema maneno yako mwenyewe ndipo utakapojifurahisha mahali pa nchi palipoinuka nitakulisha uridhi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha Bwana kimenena hayo."

Nehemia semaje kuhusu siku hii ya sabato? Imeandikwa. Nehemia 13:15, 19, 22 "Siku hiyo naliona katika Yuda watu wengine waliokanyaga mashinikizo ya mvinyo siku ya sabato, na wengine waliochukua miganda, na kuwapakia punda zao; tena na mvinyo, na zabibu na tini, na namna zote za mizigo walioyo ileta Yerusalemu, siku ya sabato nami nitakushuhudia juu ya siku ile waliyouza vyakula."

Ikawa malango ya Yerusalemu yalipoanza kuwana giza kabla ya sabato naliamuru milango ifungwe nikaamuru isifunguliwe hata sabato iishe na baadhi ya watumishi wangu nikawaweka juu ya malango, ili usiingizwe mzigo wo wote siku ya sabato."

Je! kuna ushahudi upi ya kuwa sabato iwe siku ya kuabudu?. Imeandiwa, Mambo ya walawi 23:3 "tafanya kazi siku sita; lakini siku ya saba ni sabato ya kustarehe kabisa kusanyiko takatifu; msifanye kazi ya namna yo yote ni sabato ya Bwana katika makao yenu yote."

Yesu alisema nivema kufanya jambo jema siku ya sabato. Imeandikwa, Mathayo 12:11-12 "Akawaambia nit u yupi miongoni mwenu mwenye kondoo mmoja na yule kondoo ametumbukia shimoni siku ya sabato asiyemshika akamwokoa? Je! mtu nibora kuliko kondoo mara ngapi bassi ni halali kutenda mema siku ya sabato."