Home / Masomo ya Biblia / Msongo wa Rika

Msongo wa Rika

Usijiruhusu kufafanya jambo kwa sababu ya wengine, fikiri pekeyako na uwemwangalifu. Imeandikwa, Kutoka 23:2-3 "Usiandamane na mkutano kutenda uovu wala usitie ushahidi wako katika neno lo lote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu wala usimpendele mtu mnyonge katika neno lake."

Ubaya na dhambi za pendana. Imeandikwa, Medhali 4:14-16 "Usiingie katika njia ya waovu wala usitembee katika njia ya wabaya jiepushe nayo usipite karibu nayo igeukie mbali ukaenda zako maana hawalali isipokuwa wametenda madhara huondolewa usingizi, ikiwa hawakumwangusha mtu."

Kufata watu hupotosha mtu. Imeandikwa, Mathayo 14:9 "Naye mfalme akasikitika lakini kwa ajili ya viapo vyake na kwa ajili ya wale walioketi chakulani pamoja naye akaamuru apewe, akamtuma mtu akamkata kichwa Yohana mlegerezani."

Kufanya jambo bila kufikiri huleta matokeo mabaya. Imeandikwa, Luka 23:23-24 "Lakini wakatoa sauti zao kwa nguvu sana wakitaka asulibiwe sauti zao zikashinda."

Simamia imani yako kwa Mungu bila kuwana uvuguvugu. Imeandikwa, 2Wakoritho 6:8 "Kwa utukufu na aibu kwa kunenwa vibaya na kunenwa vema kama wadanganyao bali tu watu wa kweli."