Mungu

Je! hali ya Mungu ni ya namna gani? Imeandikwa, Zaburi 145:17 "Bwana ni mwenye haki katika njia zote, na mwenye fadhili juu ya kazi zote."

Je! twaweza kumfafanua Mungu kivipi?. Imeandikwa, Kumbukumbu la torati 32:4 "Yeye mwamba kazi yake kamilifu maana njia zake zote ni haki Mungu wa uaminifu asiye na uovu yeye ndiye mwenye haki na adili."

Je! nguvu za Mungu zafika wapi?. Imeandikwa, Ayubu 36:5 "Tazama Mungu ni hodari wala hamdharau mtu ye yote ana uweza katika nguvu za ufahamu."

Je! Twaweza kumtegemea Mungu kuzishika ahadi zake?. Imeandikwa, Kumbukumbu la torati 7:9 "Basi jueni ya kuwa Bwana Mungu wenu ndiye Mungu, Mungu mwaminifuashikaye agano lake na rehema zake kwa wampendao na kuzishika amri zake hata vizazi elfu."

Mungu yuko je! Kwa neno mmoja. Imeandikwa, 1Yohana 4:8 "Yeye asiyependa hamjui Mungu kwa kuwa Mungu ni upendo."

Mungu ni mwenye rehema. Imeandikwa, Zaburi 86:15 "Lakini wewe Bwana u Mungu wa rehema na neema mvumilivu mwingi wa fadhili na kweli."

Mungu hapendelei. Imeandikwa, Matendo ya mitume 10:34-35 "Petro akafumbua kinywa chake, akasema, haki natambua Mungu hana upendeleo bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye."

Je! Mungu alienda umbali gani ili tuweze kuwa na maisha. Imeandikwa, Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee ilikila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele."

Mungu ametuonyesha upendo jinsi ulivyo. Imeandikwa 1Yohana 4:9-10 "Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu kwamba Mungu amemtuma mwanawe pekee ulimwenguni ilitupata uzima kwa yeye hili ndilo pendo si kwamba sisi tulimpenda Mungubali kwamba yeye alitupenda siss akamtuma mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu."

Yamfurahisha Mungu anapotupa neema tusiyo stahili. Imenadikwa, Mika 7:18 "Ni nani aliye Mungukama wewe mwenye kusameha uovu na kuliashilia kosa la mtu wa uridhi wake waliosalia hashiki hasira yake milele kwa maana yeye hufurahiya rehema."

Mibaraka ya Mungu haitolewi kwa wema pekee. Imeandikwa, Mathayo 5:45-46 "Ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni maana yeye huwaangazia jua wema na waovu huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki...".

Mungu anataka tuwe na vyote!. Imeandikwa, Warumi 8:32 "Yeye asiyemwashilia mwana wake mwenyewe bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote atawezaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?."
Mungu anatupenda kama baba zetu wapasavyo. Imeandikwa, 1Yohana 3:1 "Tazameni ni pendo la namna gani alilotupa Baba kwamba tuitwe wana wa Mungu na ndivyo tulivyo kwa sababu hii ulimwengu haututambui kwa kwa haukumtambua yeye."

Upendo wa Mungu nikama kimbilio. Imeandikwa, zaburi 36:7 "Ee Mungu jinsi zilivyo na dhamani fadhili zako wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako."

Twapaswa kufuata mfano wa Mungu. Imeandikwa, 1Yohana 4:11 "Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda hivi imetupasa na sisi kumpenda."

Upendo wakatimwingine wahitaji nidhamu. Imeandikwa Waebrania 12:6 "Maana yeye ambaye Bwana ampenda humrudi, hurudi naye humpiga kila mwana amkubaliye."

Mungu hatuashi na hatatuacha. Imeandikwa, Yeremia 31:3 "Bwana alinitokea zamani, akisema naam nimekupenda kwa upendo wa milele ndiyo kwa maana nimekuvuta kwa fadhili zangu."

Je! ni nini kitakasho tutenga na Mungu? Imeandikwa, Warumi 8:38-39 "Kwa maana nimekwisha kujua ya kwamba wala mauti wala uzia, wala malaika wala wenye mamlaka, wala yaliopo wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo wala yaliyo juu wala yaliyo chini wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu."