Neno

Maneno yetu ya mtukuze Mungu. Imeandikwa, Zaburi 19:14 "Maneno ya kinywa changu na mawazo ya moyo wangu yapate kibali mbele zako, Ee BWANA, Mwamba wangu, na Mwokozi wangu."

Neno lina nguvu. Wakati mwingine ni vema kuwa kimya. Imeandikwa, Mithali 13:3 "Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake bali afunuaye midomo yake atapata uharibifu."

Maneno yetu yaonyesha jinsi tulivyo. Imeandikwa, Mathayo 12:34 "Enyi wazao wa nyoka mwa wezaje kunena mema mkiwa wabaya? maana kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake."

Maneno yetu ni ya muhimu kwani sisi tulio wakristo. Imeandikwa, Wakolosai 4:6 "Maneno yenu yawe na neema siku zote yakikolea munyu mpate kujua jinsi iwapasavyo kujibu kila mtu."

Je! twapaswa maneno yetu yawe juu ya nini? Imeandikwa. Waefeso 5:4 "Wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi hayo hayapendezi bali afadhali kushukuru."

Maneno yetu yaweza kuwasaidia watu katika maisha yao. Imeandikwa, Mithali25:11 "Neno linenwalo wakati wa kufaa ni kama machunzwa katika viano vya fedha." Isaiya 50:4 yasema "Bwana Mungu amenipa ulimi wa hao wafundishwao nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka huniamsha asubuhi baada ya asubuhi huniamsha sikio langu lipate kusikia kama watu wafundishwao".

Mojawapo ya amri za Mungu inakataza kulitumia jina la Mungu bure. Imeandikwa Kutoka 20:7 "Usilitaje bure jina la BWANA Mungu wako maana BWANA hatamhesabia hana hatia mtu alitajaye jina lake bure."