Utii

Kutii Mungu ni bora kwetu. Imeandikwa, Kubukumbu la torati 30:15-16 "Anagalia niekuwekea mbele yako uzima na mema na mauti na mabaya kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda Bwana, Mungu wako kuenenda katika njia zake na kushika maagizo yake na amri zake na hukumu zake upate kuwa hai na kuongezeka; Bwana Mungu wako, apatekukubariki katika nchi uingiayo kuimiliki." Kumbukumbu la torati 10:12, 13 yasema "Na sasa, Bwana Mungu wako anataka nini kwako, ila kwenda katika njia zake zote, kumpenda na kumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote kuzishika amri za Bwana na sheria zake ninazo kuamuru leo upate uheri."

Je! sheria, neema na kutii zina shirikianaje. Warumi 5:20 "Sheria iliingia ili kosa liwe kubwa sana na dhambi ilipozidi neema ilikuwa nyingi zaidi."

Kutii kwa weza kutuokoa katika magonjwa. Imeandikwa, Kutoka 15:26 "Akawaambia kwamba, utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia wamisri kwa kuwa mimi ndimi Bwana Mungu wako ni kuponyaye."

Kutii ni ufunguo wa kufanikiwa. Imeandikwa, Yoshua 1:8 "Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku upate kuangalia kutenda sawa sawa na maneno yote yaliloandikwa humo maana ndipoutakapofanikisha njia yako kisha ndipo utakapostawi sana."

Tutahukumia kutoka na utiifu wa sheria za Mungu. Imeadikwa. Mathayo 5:19 "Basi mtu ye yote atakaye vunja amri moja katika zilizo ndogo na kuwafundisha watu hivyo ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni bali mtu atakaye zitenda na kuzifundisha huyo ataitwa mkuu katika ufalme wa mbinguni."

Kutii nionyesho la kumpenda Mungu. Imeandikwa, Yohana 14:15 pia 23 "Mkinipenda mtazishika amri zangu. Yesu akajibu akawaabia, mtu akinipenda atalishika neno langu, na baba yangu atampenda nasi tutakuja kwake na kufanya makao kwake."

Roho mtakatifu atamwagiwa wale wanao tii Mungu. Imeandikwa, Matendo ya mitume 5:32 "Na sisi tumashahidi wa mambo haya pamoja na Roho takatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio."

Yesu alitii Baba yeke mfano kwetu tunavyo paswa kumtii Mungu. Imeandikwa, Waebrania 5:8-9 "Na ingawa ni Mwana alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyo mpata, naye alipokwisha kukamilishwa akawa sasbu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii."

Mungu ametushauri kutii sheria za nchi. Imeandikwa, Warumi 13:1-2. "Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu kwa maana hakuna mamlaka isiyo toka kwa Mungu na ile iliyoko ueamuriwa na Mungu. Hivyo amwasiye wenye malaka hushindana na agizo la Mungu nao washindanao watajipata hukumuni."

Wakati mwingin enivema kumtii Mungu kuliko kutii sheria za nchi. Imeandikwa, Matendo ya mitume 5:29 "Petro na mitume wakajibu wakisema, imetupasa kumtii Mungu kuliko kumtii mwanadamu."

Watoto wawatii wazazi wao. Imeandikwa, Waefeso 6:1-3 "Enyi watoto watiini wazazi wenu katika Bwana maana hii ndiyo haki. waheshimu baba yako na mama yako amri hii ndiyo ya kwanza yenye ahadi upate heri ukae siku nyingi katika dunia."