Home / Masomo ya Biblia / Anayesimama mahali pa Kristo

Anayesimama mahali pa Kristo

Mungu anatueleza jinsi itakavyo kuwa kwa wale ambao wanaoishi katika nyakati za mwisho. Imeandikwa. 1Yohana 2:18 " Watoto ni wakati wa mwisho; na kama mlivyo sikia kwamba mpinga Kristo yuaja hata sasa wapinga kristo wengi wame kwisha kuwapo kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho."

Neno la asili la Kiyunani la "anaye mpinga Kristo" laweza kuwa na maana mbili. Laweza kumaanisha 'aliye kinyume na Kristo', kwa maana ya mtu au mamlaka ipingayo kazi ya Kristo. Au kwa matumizi mengine, neno hilo laweza kumaanisha 'badala ya Kristo', likimaanisha mtu au mamlaka ichukuayo 'mahali pa Kristo', au ni 'Kristo bandia'. Mungu anasema ya kwamba zaidi ya kuja kwa Mpingakristo halisi, walikuwapo wapingaKristo wengine wengi tayari wakati wa kanisa la awali la kikristo. Imo katika Biblia, 1Yohana 2:19, 26 "Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalika pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu. 26 "Nimewaandikia haya katika habari za watu wale wanaotaka kuwa poteza."

Katika maandiko, wanao mpinga kristo walitoka katika imani ya kweli wao ambao walikataa habari za Yesu. Imo katika Biblia, 1Yohana 2:22 "Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpiga kristo, yeye amkanaye baba na mwana." 2 Yohana 1:7 "Kwa maana wadanganyifu wengi wame toka duniani, wasiyo kiri ya kuwa Yesu kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye mdanganyifu na mpinga kristo."

Wapinga Kristo sio wale ambao hawamjui Kristo wala watu wa nje wasio na dini kumfanyia vita yeye Yesu bali ni hao ambao wanaofunza au kuhubiri injili, lakini niya kupotosha au injili tofauti na ile ya haswa. 2Wakorintho 11:4, 13-15 "Maana yeye ajaye akihubiri Yesu Mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea au injili nyingine msiyoikubali mnatenda vema kuvumilia naye." 13-15 "Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watenda kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu. maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kuwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao."

Yesu alilionya kanisa lake kuhusu makristo wa uwongo. Imo katika Biblia, Mathayo 7:15, 21-23 "Jihadharini na manabii wa uongo watu wanowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa wa mwitu wakali. 21-23, Si kila mtu aniambiaye Bwana, Bwana atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu." Yesu alilionya kanisa lake kuwa kitambo kidogo kabla ya kuja kwake mara ya pili yule anayempinga Kristo atajaribu kufanana naye Yesu hasa kuwaambia watu kuwa yesu amerudu mara ya pili Imeandikwa Mathayo 24:4, 5, 24-26 "Yesu akajibu, akawaambia angalieni mtu asiwadanganye. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi. 24-26 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. Basi wakiwaambia yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki." 2 Wathesalonike 2:3 - 4 "Mtu awayeyote asiwadangaye kwa njia yo yote maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu, ama kuabudiwa hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu."

2 Wathesalonike 2:8-10 "Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambapo Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake; yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake shetani kwa uwezo wote na ishara na ajabu za uongo na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanao potea kwa sababu hakuipenda ile kweli wapate kuokolewa."