Home / Masomo ya Biblia / Kufikiri

Kufikiri

Fikiri kabla hujanena na kuonyesha kutokujua kwako. Imeandikwa, Mithali 15:28 "Moyo wa mwenye haki hufikiri atakavyojibu bali kinywa cha wasio haki humwaga mabaya."

Lazima tuwe na nidhamu katika mafikara yetu na kufikiri mambo mema kwani hapo ndipo chanzo cha mambo yote. Imeandikwa, Marko 7:21-22 "Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya na uasherati. wivu, uuaji, uzinzi, tama mbaya ukorofi, hila, ufisadi, kijicho matukano, kiburi, upumbavu." Mithali 23:7 sayema "Maana aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo. akauambia, haya, kula, kunywa, lakini moyo wake hauwi pamoja nawe."

Baada ya kumkubali Yesu yatupasa tumpe nafasi Roho mtakatifu abadili mawazo yetu. Imeandikwa Warumi 12:2 "Wala msiifuatishe nana ya dunia hii bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema ya kumpendeza, na ukamilifu."

Lazima tufikiri mambo mema ndipo maneno yetu na matendo yetu yawe ya busara na yenye kusaidia. Imeandikwa, Wafilipi 4:8 "Hatimaye ndugu zangu mambo yo yote yaliyo ya kweli yo yote yaliyo staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema, ukiwapowema wo wote ikiwapo sifa nzuri yo yote, ya tafakarini hayo."

Tuwe na mafikara kama ya Kristo. Imeandikwa Wafilipi 2:5 "Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu."