Home / Masomo ya Biblia / Uvumilivu

Uvumilivu

Uvumilivu wetu wazezaje kutothohofika? Uvumilivu hukuwa kwa dhiki na kwa wakti mgumu. Imeandikwa, Warumi 5:3 "Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia mkijua yakuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi." Yakobo 1:3-4 "Mkifahamu yakuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno."

Uvumilivu wetu u sabamba na imani yetu na Mungu. Imeandikwa, Ufunuo 14:12 "Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu."

Watu wa Mungu wavumiliane. Imeandikwa, Wefeso 4:2 "Kwa unyenyekevu wote na upole kwa uvumilivu mkichukuliana katika upendo."

Wenye uvumilivu wamebarikiwa na ahadi ya Mungu. Imeandikwa, Webrania 6:12 "Ili msiwe wavivu bali mkawe wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imani ya uvumilivu."

Tuwe wavumilivu kwa kuja kwa Yesu. Imeandikwa, Yakobo 5:7-8 "Kwa hiyo ndungu vumilieni hata kwa kuja kwake Bwana tazama mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya dhamani huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho nanyi mvumilieni mthibitishe mioyo yenu kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia."