Home / Masomo ya Biblia / Kutumainiwa

Kutumainiwa

Twaweza kumtumaini Mungu kwakuwa hi nitabia yake. Imeandikwa, Zaburi 33:4 "Kwa kuwa neno la Bwana lina adili, na kazi yake yote hutenda kwa uaminifu." Waebrania 13:5 yasema "Msiwe na tabia ya kupenda fedha mwe radhi na vitu mlivyo navyo kwa kuwa yeye mwenyewe asema sita kupungukia kabisa wala sita kuacha kabisa."

Wakristo wapswa kuaminiwa wakati wote. Imeandikwa, Waefeso 4:15-16 "Lakini tuishike katika upendo na kukua hat tumfikie yeye katika yote yeyee aliye kichwa Kristo... katika yeye mwili wote ukiugamanisha na kushikanishwa kwa msaada kwa kila kiungo kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja huukuza mwili upate kujijengea wenyewe katika upendo."

Wokovu ni kwa wale waaminifu. Imeandikwa, Mathayo10:22 "Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwaajili ya jina langu lakini mwenye kuvumilia hata mwisho ndiye atakayeokoka."

Mungu anataka watu waminifu. Imeandikwa, Mathayo 24:45 "Ni nani basi yule mtumwa mwamini mwenye akili ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake awape watu wake chakula kwa wakati wake."

Mungu ametuahidi kuwa mwamini kwetu hata kufa. Imeandikwa, Ufunuo 2:10 "Usiogope mambo yatakayokupata tazama huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe nanyi mtakuwana dhiki siku kumi. Uwe mwamini hata kufa nami nitakupa taji ya uzima."