Mungu anatutazamia tu tunze ahadi zetu. Imeandikwa, Mambo ya walawi 5:4 "Au kama mtu akijiapisha kwa kutamka haraka kwa midomo yake kutenda uovu au kutenda mema neno lo lote mtu atakalo litamka kwa kiapop pasipo kufikiri na neno hilo likamfiachamania hapo atakapolijua ndipo atakapokuwa na hatia katika mambo hayo mojawapo."
Munug anachukulia ahadi zetu kw ahali ya juu. Imeandikwa, Mithali 20:25 "Ni mtego mtu aseme kwa haraka kitu hiki ni wakfu na baadaya kuweka nadhiri kuuliza -uluza habari."
Yesu alieleza umuhimu wa kutimiza ahadi zetu. Imeandikwa, Mathayo 5:37 "Bali maneno yenu yawe ndiyo, ndiyo, siyo siyo kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu."
Ahadi ambazo zimeahidikwa kwa Mungu lazima zitimizwe kwa upesi. Imeandikwa, Mhubiri 5:4-5 "Wewe ukimwekea Mungu nadhiri usikawiye kuiondoa kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu basi uiondoe hiyo radhi uliyoiweka nadhirini afadhali usiweke nanadhiri kuliko kuiweka usiiondoe."
Ahadi za ndoa ni za milele. Imeandikwa, Mathayo 19:5-6 "Akasema kwa sababu hiyo mtu atamwacha babayake na mamayake ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja hatawamekuwa si wawili tena bali mwili mmoja basi aliyewaunganisha Mungu mwanadamu asiwatenganishe."