Udhuru

Kusingizia kulianza hapo mwanzo wa dhambi Imeandikwa Mwanzo 3:11-13 "Akasema ni nani aliyekwambia ya kuwa u uchi? je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokwagiza usiyale? Adamu akasema huyo mwanamke uliyonipa awepamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mtu huo nikala Bwana Mungu akamwambia mwanamke, nini hilo ulilolifanya? Mwanamke akasema nyoka alinidanganya nikala."

Usiwe na singizio unapoomba msamaha wa dhambi zako. Imeandikwa Yakobo 1:13-15 "Mtu ajaribiwapo asiseme ninajaribiwa na Mungu maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutuwa na kudanganywa halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi na ili dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti."

Usitafute kizingizio kutoka katika ndoa Imeandikwa Mathayo 5:32 " Lakini mimi nawaambia kila mtu amwachaye mkewe isipokuwa kwa habari ya usherati amefanywa kuwa mzinzi na mtu akimuoa yule aliyeachwa azini."

Wakati Mungu anatupatia maagizo anakusudia tushirikiane na wala sikuwa na masingizio. Atatutimizia yote tunayo hitaji. Imeandikwa Kutoka 4:10-12 "Musa akamwambi Bwana ee Bwana mimi si msemaji tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako maana mimi si mwepesi wa kusema na ulimi wangu ni mzito Bwana akamwambia ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani afanyaye mtu kuwa kiziwi au bubu au mwenye kuona au kuwa kipofu si mimi Bwana? basi sasa enenda nami nitakuwa pamoja na kinywa chako na kukufundisha utakalolisema."

Tusiwe na vizingizio tunapoitwa na Mungu. Imeandikwa Luka 14:15-24. "Basi aliposikia hayo mmojawapo wa wale waliketi chakulani pamoja naye alimwambia, heri yule atakaye kula mkate katika ufalme wa Mungu akamwambia mtu mmoja alifanya karamu akaalika watu wengi akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, njoni kwa kuwa vitu vyote vimekwicha kuwekwa tayari wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. wakwanza alimwambia nimenunua shamba shari niende nikalitazame tafadhali nisamehe mwingine akasema nimenunua ngo'mbe jozi tano nimekwenda kuwajaribu tafadhali nisamehe. Mwingine akasema nimeoa na kwasababu hiyo siwezi kuja yule mtumwa akaenda akmpa habari bwana wake habari ya mambo hayo. Basi yule mwenye nyumba akakasirika akamwambia mtumwa wake toka upesi uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini na vilema, na vipofu na viwete mtumwa akasema hayouliyoagiza yamekwicha tendeka na hata sasa ingaliko nafasi Bwana akamwambia mtumwa toka nje uende barabarani na mipakani ukawashurutishe kuingia ndani nyumba yangu ipatekujaa. Maana na waambia ya kwamba katika wale walioalikwa hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu."