Fedha

Je mibaraka mali yatoka wapi? Imeandikwa, Kumbukumbu la torati 8:18 "Bali utamkumbuka Bwana Mungu wako maana ndiye akupaye nguvu zakupata utajiri ili alifanye agono lake alilowapa baba zako kama hivi leo."

Je pesa zaweza kuchukua mahala pa mambo yaliyo bora?. Imeandikwa, Yeremia 9:23-24 "Bwana asema hivi mwenye hekima asijisifu kwa hekima yake wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake wala tajiri asijisifu kw a sababu ya utajiri wake bali ajisifuye ajisifu kwa sababu hii ya kwamba ananifahamu mimi na kunijua ya kuwa mimi ni Bwana nitendaye wema na hukumu na haki katika nchi maana mimi napendezwa na mabo hayo asema Bwana."

Mali yaweza kutupa mfano mbaya juu ya vitu. Imeandiikwa, Luka 12:15 " Yesu akawaambia angalieni, jilindeni na choyo maana uzima wa mtu haumo katika vitu vyake alivyo navyo."

Nivibaya kuweka pesa mbele ya vitu vingine vyote. Imeandikwa, Mathayo 6:24 "Hakuna mtu awezaye kuwatumikia mabwana wawili kwa maana atamchukia huyu na kumpenda huyu na ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu hamwezi kumtumikia Mungu na mali." 1 Timotheo 6:9 "Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi na tamaa nyingi zisizo na maana zenye kudhuru ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu."

Nivigumu tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni. Imeandikwa, Marko 10:23-25 "Yesu akatazama kotekote akawaambia wanafunzi wake jinsi itakavyokuwa shinda mwenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu wana funzi wakachangaa kwa maneno yake Yesu akajibu tena akawaamabia, watoto jinsi ilivyo shida mwernye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu ni rahisi ngai akupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu."

Kupenda pesa huleta dhambi. Imeandikwa, 1Timotheo 6:10 "Maana shina moja ya mabaya ya kila namna ni kupenda fedhaamabayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na imani na kujichoma kwa maumivu mengi."

Kutosheka sikuwana mali au fedha nyingi. Imeandikwa, Wafilipi 4:12-13 "Na jua kudhiliwa tena na jua kufanikiwa katika hali yo yote katika mambo yo yote niefundishwa kushiba na kuona njaa kuwa na vingi na kupungukiwa na yaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu."

Imeandikwa Mathayo 6:21 "Kwa kuwa hazina yako ilipo ndipo utakapokuwapo moyo wako."