Home / Masomo ya Biblia / Huduma ya Uoshaji Miguu

Huduma ya Uoshaji Miguu

Yesu alionyeshakuwa ni muhimu kuosha miguu kabla ya pasaka. Imeandikwa, Yohana 13:4-17 "Yesu, aliondoka chakulani akaweka kando mavazi yake akatwaa kitambaa akajifunga kiunoni, kisha akatia maji katika bakuli akaanza kuwatawadha wanafunzi minguu na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga. Hivyo yuaja kwa Simoni Petro, huyo akamwambia Bwana! wewe wanitawadha minguu mimi? Yesu akajibu akamwambia nifanyalo wewe hujui sasa lakini utalifahau baadaye akamwambia wewe hutanitawadha miguu mimi kamwe Yesu akamwambia kama nisipokutawadha huna shirika nami Simoni petro akamwambia Bwana si minguu yangu tuu hata na mikono na kichwa changu pia. Yesu akawambia yeye liye kwicha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu bali yu safi mwili wote nanyi mmekua safi lakini si nyote kwa maana alijua yeye atakaye msaliti ndiyo maana alisema si nyote mlio safi. Basi alipokwisha kuwatawadha miguu na kuyatwaa mavazi yake na kuketi tena akawaambia je! Mmeelewa na hayo niliyoyatenda? nanyi mwaniita mwalimu na, Bwana nanyi mwa nena vyema maana ndivyo nilivyo. Basi ikawa mimi niliye Bwana na mwalimu nimewatawadha miguu imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi kwa kuwa nimewapa kielezo ilikama mimi nivyo watendea nanyi mtende vivyo. Amini amini nawaambia ninyi tumwa simkuu kuliko Bwana wake wala mtume si kuu kuliko aliyempeleka. Mkiyajua hayo heri ninyi akiyatenda."