Kukuwa

Ukuwaji wa kiroho ndio nia ya mkristo imeandikwa 2 Petro 3:18 "Lakini kueeni katika neema na katika kumjua Bwana wetu na mwokozi Yesu Kristo. Utukufu unayeye sasa na hata milelel."
Lazima tuwe na nidhamu ikiwa tutataka kukuwa kiroho. Imeandikwa 1 Wakorintho 9:25 "Nakila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; badi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo bali sisi tupokee taji isiyoharibika."

Tutazidi kukuwa kiroho hadi Yesu atakaporudi. Imeandikwa Wafilipi 1:6 "Nami niliaminilo ndilo hili yakwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Yesu Kristo."

Kukuwa kiroho kwahitaji mazoezi. Imeandikwa Waebrania 5:12-14 " Kwa maana iwapasavyo waalimu, maana wakati mwingi umepita mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu ninyi mmekuwa mnahitaji maziwa si chakula kigumu. kwaama kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki kwa kuwa ni mtoto mchanga lakini chakula kingumu ni cha watu wazima ambao akili zao kwa kutukiwa zimewezwa kupambanua mema na mabaya."