Home / Masomo ya Biblia / Kutokuoa

Kutokuoa

Kuolewa na kutoolewa ni baraka kutoka kwa Mungu. Imeandikwa, 1Wakorintho 7:6-7 "Lakini nasema hayo kwa kutoa idhini yangu si kwa amri ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo walakini kila mtu ana karama yake itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi."

Wakati mwema wa kukaa bila kuoa ni kuweza kuwa na mda wa kumtumikia Mungu. Imeandikwa, 1Wakorintho 7:29-31 "Lakini ndungu nasema hivi muda ubakio si mwingi basi tokea sasa wale walio na wake na wawe kama hawana na wale waliao kama hawalii na wale wafurahio kama hawafurahi na wale wanunuao kama hawana kitu na wale wautumiao ulimwengu huu kama hawautumii sana kwa maana mambo ya ulimwengu huu yatapita."