Nidhamu

Nidhamu ni matunda ya upendo imeandikwa Waebrania 12:5-11 "Tena mmeyasahau yale maonyo yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu usiyadharau marudia ya Bwana wala usizimie moyo ukikemewa naye maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi naye humpiga kila mwana amkubaliye ni kwa ajili ya kurudiwa mwahistahimili, Mungu awatendea kama wana maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? Basi kama mkiwa hamna kurudiwa ambako ni fungu la wote ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi wala si wana wa halali. na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si hafadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu za kuishi? Maana ni hakika wao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe bali yeye kwa faida yetu, ili tushiriki utakatifu wake. Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha bali cha huzuni lakini baadaye huwaletea wao waliozoelezwa nayo matunda ya haki yenye amani."

Nidhamu ni maonyesho au matunda ya upendo wa wazazi. imeandikwa Medhali 13:24 "Yeye asiye tumia fimbo yake humchukia mwanawe; bali yeye ampendaye humrudi mapema."

Ukimpa nidhamu mtoto akiwa mdogo utaondoa shidaningi katika siku zijazo. Imeandikwa Medhali 19:18 "Mrudi mwanao, kwa maana liko tumaini; wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake."