Home / Masomo ya Biblia / Shukurani

Shukurani

Anza siku kwa kushukuru. Imeandikwa, Zaburi 92:1-2 "Ni neno jema kumshukuru Bwana na kuliimbia jina lako Ee uliye juu kuzitangaza rehema zako asubuhi na uwaminifu wako wakati wa usiku."

Dalili ya kumasha Mungu nikukosa kumshukuru. Imeandikwa, Warumi 1:21 "Kwa sababu walipo mjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru bali walipotea katika uzushi wao na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza."

Mshukuru Mungu kwa kila jambo. Imeandikwa, 1Wathesalonike 5:18 "Shukuruni kwa kila jambo maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Yesu Kristo."

Tunapo mshukuru Mungu tusisahau mibaraka yetu itokapo. Imeandikwa, Zaburi 103:2 "Ee nafsi yangu mhimidi Bwana wala usizisahau fadhili zake zote."