Sifa njema ni heri kuliko mali. Imeandikwa, Mithali 22:1 "Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi na neema kuliko fedha na dhahabu."
Waweza kuharibu sifa yako kwa kufanya jambo lisilo jema. Imeandikwa, Mithali 25:9-10 "Ujitetee na mwenzako peke yake bali usifunue siri ya mtu mwengine. Yeye asikiaye asije akakutukana na aibu yako isiondoke."
Je! nimambo gain yanayo leta sifa njema?. Imeandikwa, Mithali 22:4 "Macho yenye kiburi na moyo wa kutabakari hata ukulima wa waovu, ni dhambi."
Wema huleta heshima. Imeandikwa, Mithali 11:16 "Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima Na watu wakali mali siku zote."
Nivema kuwa na sifa njema katika mahala pa kazi. Imeandikwa, Mithali 22:29 "Je! Mwaona mtu mwenye bidii katika kazi zake? huyo atasimama mbele ya wafalme hatasimamana mbele ya watu wasio na cheo."