Home / Masomo ya Biblia / Uhusiano

Uhusiano

Uhusiano wetu na wengine usididimishe imani yetu. Imeandikwa, 2 Wakorintho 6:14 "Msifungwe nira pamoja na wasio amini kwa jinsi isivyo sawasawa kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?."

Uhusiano wetu na wengine waimarishwa kupitia kwa Yesu. Imeandikwa, Waefeso 2:21-22 "Katika yeye jingo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskini ya Mungu katika Roho."

Tutakuwa kama watu tunoshirikiana nao. Imeandikwa, Mithali 13:20 "Enenda pamoja na wenye hekima nawe utakuwa na hekima bali rafiki wa wapumbavu ataumia."