Je bibilia yasema nini kuhusu mapenzi ya namna hii? Imeandikwa, Warumi 1:26-27 "Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tama zao za aidu hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasio ya asili wanaume nao vivyo hivyo, waliyaacha mtumizi ya mke, ya asili wakawakiana tama wanaume wakayatenda yasiyopasa wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao."
Je! mapenzi ya namna hii ni dhambi? Imeandikwa, Mambo ya walawi 18:22 "Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke ni machukizo."
Je anayefanya mapenzi ya namna hii atauridhi uzima? Imeandikwa, 1Wakorintho 6:9 "Au hamjui yakuwa wadhalimu hawatauridhi ufalme wa Mungu wala wabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti."
Kama watenda dhambi wengine wanao fanya mapenzi ya namna hii wameitwa kutubu dhambi zao. Imeandikwa, 1Timotheo 1:10-11 "Na wazinzi, na wafiraji, na waibao watu, na waongo nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana mafundisho yenye uzima, kama vile ilivyo nenwa katika habari njema ya utukufu wa Mungu ahidimiwaye, niliyowekewa amana."
Dhambi yaaina yo yote itupiliwe mbali na tuombe msamaha kwa Mungu. Imeandikwa, 1 Wakorintho 6:11 "Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii, lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo na katika Roho wa Mungu wetu."
Kuna tumaini kwa wao watendao mapenzi ya namna hii. Imeandikwa, 1Wakorintho 10:13 "Jaribu halikuwapata ninyi isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu ila Mungu ni mwaminifu ambay hatawaachamjaribiwe kupita mwezavyo lakini paoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ilimweze kustahimili."
Je! kama wanfanya mapenzi ya namna hii ufanye je?. Kwanza kubali dhambi zako. Imeandikwa, Zaburi 51:2-4 "Unioshe kabisa na uovu wangu unitakase dhmbi zangu... maana nimeyajua mimi makosa yangu "
Pili omba msamaha kwa Mungu. Imeandikwa, Zaburi 51:7-12 "Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, unioshe nami nitakuwa mweupe kuliko theluji unifanye kusikia furaha na shangwe mifupa uliyoiponda ifurahi. Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; uzifute hatia zangu zote. Ee Mungu uniumbie moyo safi, uifanye upia roho iliyotulia ndani yangu. Usinitenge na uso wako wala Roho yako mtakatifu usiniondolee. Unirudishie furaha ya wokovu wako unitegemeze kwa roho ya usafi."
Tatu kubali yakuwa Mungu amekusamehe dhambi zako. Imeandikwa Zaburi 32:1-6 "Heri aliyesamehewa dhambi, na kusitiriwa makosa yake. Heri Bwana asiyemhesabia upotovu,, ambaye rohoni mwake hamna hila. Niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa kwa kuugua kwangu mchana kutwa kwa maana mchana na usiku mkono wako ulinilemea. jasho langu likakauka hata nikawa kama nchi kavu wakati wa kaskazi. Nalikujulisha dhambi yangu wala sikuufisha upotovu wangu nalisema nitayakiri maasi yangu kwa Bwana nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu. Kwa hiyo kila mtu mtauwa akuombe wakati unapopatikana, hakika maji makuu ya furikapo hayatamfikia yeye."