Home / Masomo ya Biblia / Umaskini

Umaskini

Pesa sio kila kitu. Imeandikwa, Mithali 13:7-8 "Kuna mtu mwenyekujitajirisha, lakini hana kitu kuna ajifanyaye kuwa maskini lakini anamali nyingi dia ya nafsi ya mtu ni utajiri wake, bali mtu maskini hasikii ogofyo lo lote."

Usistaajabi watu wakiwapa matajiri heshima, kwani Mungu atampaheshima maskini. Imeandikwa, Yakobo 2:5 "Ndugu zangu wapenzi sikilizeni, je! Mungu huwachagua maskini wa duni a wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?".

Tuweni na moyo wakuwasaidia maskini. Imeandikwa, Wagalatia 2:10 "Ila neno moja tuu walitutakia tuwakumbuke maskini nami neno lilo hilo nalikuwa na bidii kufanya."

Kutowasaidia wenye mahitaji ni dhambi. Imeandikwa, Amosi 5:12 "Maana mimi najua maasi yenu yalivyo mengi na jinsi dhambi zenu zilivyo kubwa ninyi mnaowaonea wenye haki mnaopokea rushwa na kuwageuza wahitaji langoni wasipate haki yao."

Kusaidia maskini huleta mibaraka kwa Mungu. Imeandikwa, Zaburi 41:1 "Heri akumbukaye mnyonge Bwana atamwokoa siku ya taabu."

Twamuhesshimu Mungu kwa kuwasaidia maskini. Imeandikwa, Mithali 14:31 "Amwonaye maskini humsuta uumba wake. Bali yeye awahurmiaye wahitaji humheshimu."

Kanisa lapaswa kuwasaidia watu wenye shida na wasio na jamii. Imeandikwa, 1Timotheo 5:5-6 "Basi yeye aliye jane kweli kweli, ameachwa peke yake huyo amemwekea Mungu tumaini lake, naye hudumu katika maombi na sala mchana na usiku. Basi, yeye asiye jizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai."

Mungu amewaahudi watu wanao wasaidia maskini na wasio jiweza. Imeandikwa, Isaya 58:7-11 "Je! siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako na kuwaleta maskini waliotupwa nyumbani mwako? uwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo wal usijifishe na mtu mwenye damu moja nawe? ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi na afya yako itatokwea mara na haki yako itakutangulia utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde ndipo utaita na Bwana ataitika, utalia naye atasema, mimi hapa. kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako wala kunyosha kidole wala kunena maovu na kama ukimkunjia mtu mwenye njaa nafsi yako na kuishibisha nafsi iliyoteswa ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri naye Bwana atakuongoza daima ataishibisha nafsi yako mahala pasipokuwa na maji na kuitia nguvu mifupa yako nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui."

Tuwe kwa niaba ya maskini. Imeandikwa, Amosi 5:24, "Lakini hukumu na iteleke kama maji, na haki kama maji makuu."