Ahadi

Mungu anahitaji tutimize ahadi zetu. Imeandikwa, Hesabu 30:1-2 "Kisha Musa akanena na wale vichwa vyakabila vya wana wa Israeli na kuwaambia neno hili ndilo alizoliagiza Bwana mtu akapomweka Bwana nadhiri au atakapo kiapa ili kufunga nafsi yake kwa kifungo asilitangue neno lake atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake."

Usikawiye kutimiza ahadi yako kwa Mungu. Imeandikwa, Mhubiri 5:4-5 "Wewe ukimwekea Mungu nadhari usikawiye kuiondoa kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu basi uiondoe hiyo uliyoiweka nadhari ni afadhali usiwe na nadhiri kuli kokuiweka usiiondoe."

Mungu hutimiza ahadi zake. Imeandikwa, 2Wakorintho 1:19-20 "Maana mwana wa Mungu kristo Yesu aliyehubiriwa katikati yenu na sisi yani mimi na siliwano na Timotheo hakuwa ndiye na siyo bali katika yeye ni ndiyo maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni ndiyo ten akwa hiyo katika yeye ni amin. Mungu apate kutukuzwa kwa sisi."

Mungu hazirudishi ahadi zake au kuzibadili. Imeandikwa, Zaburi 89:34 "Mimi sitalihalifu agano langu sitalibadili neno lililotoka midomoni mwangu."

Hakuna ahadi ya Mungu ambayo hakutimia. Imeandikwa, Yoshua 23:14 "Angalieni mimi leo ninakwenda njia ile waendayo watu wote waulimwengu nanyi nyote mwajua mioyoni mwenu na rohoni mwenu yakuwa haikuwapungukia ninyi hata neno moja katika mambo hayo mema yote aliyo yanena Bwana Mungu wenu katika habari zenu; yote yametimia kwenu hapana neno lo lote mlilopungukiwa."