Home / Masomo ya Biblia / Asiye jiweza

Asiye jiweza

Kwake Yesu viwete walikuwa wa kuonyesha utukufu wa Mungu imeandikwa Yohana 9:2-3 "Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema niyupi aliyetenda dhambi mtu huyu au wazazi wake hata azaliwe kipofu? Yesu akajibu huyu hakutenda dhambi wala wazazi wake bali kazi ya Mungu zidhihiriswe ndani yake."

Mipaka yetu si ya milele imeandikwa 1Wakorintho 15:53 " Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika nao huu wa kufa uvae kutokufa."

Viwete wata ponywa imeandikwa Isaya 35:5-6 " Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya visiwi yatazibuliwa ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu na ulimi wake aliye bubu utaimba maana katika nyika maji yata bubjika na vijito janguani."