Bishana

Kuna ubaya gani kubishana. Imo katika Biblia, Wafilipi 2:14 "Yatendeni mambo yote pasipo manung'unuko wala mashindano".

Usipoteze muda wako kubishania mambo yasiyo na umaana. Imo katika Biblia, Tito 3:9 "Lakini maswali ya upuzi jiepushe nayo, na nasaba na magomvi na mashindano ya sheria. Kwa kuwa hayana faida tena hayana maana."

Fikiria kabla huja nena neno. Imo katika Biblia, Mithali 15:28 "Moyo wa mwenye haki hufikiri jinsi atakavyojibu; Bali kinywa cha wasio haki humwaga mabaya."

Jibu kwa utulivu kuzuia mabishano. Imo katika Biblia, Mithali 15:1 "Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu."

Je? Ni vema kujiingiza kati yao wanaobishana? Mithali 26:17 "Mtu apitaye na kujisumbua kwa ugomvi usio wake; Ni kama mtu ashikaye mbwa kwa masikio yake."