Hifadhi

Twaweza kumtegemea Mungu kutuhifadhi. Imeandikwa, Zaburi 18:2 Bwana ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu mwamba wangu ninayemkimbilia ngao yangu na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu."

Wafuasi wa Yesu hawataangamia milele. Imeandikwa, Luka 21:17-19 "Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu walakini hatutapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu."

Mungu yuko tayari kutusaidia. Imeandikwa, Zaburi 46:1-3 "Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu saada utakaoonekana tele wakati wa mateso kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. maji yake yajapovuma na kuumuka ijapopepesuka milima kwa kiburi chake."

Mungu hajatuahidi aisha bila taabu, bali ameahidi kuwa nasi katika shida na dhiki. Imeandikwa, Zaburi 91, Aketiye mahali pasiri pake aliye juu atakaa katika uvuli wake mwenyezi nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayetumaini maana yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji na katika tauni iharibuyo. kwa manyoya yake atakufunika chini ya mbwa zake utapatakimbilio uaminifu wake ni ngao na kigao. hutaogopa hofu ya usiku, wala mchale urukao mchana wala tauni ipitayo gizani wala uele uharibio adhuhuri.

Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako naam kumi elfu mkono wako wa kuume hatahivyo hautakukaribia wewe ila kwa macho utatazama na kuyaona malipo ya wasio haki kwa kuwa wewe Bwana ndiwe kimbilio langu umefanya aliye juu kuwa makao yako. Mabaya hayatakupata wewe wala tauni haitakaribia hema yako kwa kuwa atakuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote. mikononi mwao watakuchukua, usije ukajigwaa mguu wako katika jiwe utawakanyaga siba na nyoka, wana simba na joka utawaseta kwa miguu. Kwa kuwa amekaza kunipenda nitamwokoa; na kumweka katika juu, kwa kuwa amenijua jina langu.

Ataniita nami nitawitikia nitakuwa pamoja naye taabuni, nitamwokoa na kumtukuza, kwa siku nyingi nitamshibisha nami nitamwonyesha wokovu wangu."