Home / Masomo ya Biblia / Jiwe la kioo

Jiwe la kioo

Watu wengi wana imani yakuwa kana jiwe ambalo huwaletea nguvu zisizo za kawaida ambayo ya weza kutumika kwa uponyaji. Pia wana amini yakuwa jiwe au aina ya mawe Fulani yaweza kuwasaidia kukuwa katika hali ya kiroho ambayo huleta matokeo mema katika hali ya maisha. Utumiaji wa mawe haya yalikuwa yakifanywa watu asio mwamini Mungu wakati wa zamini na enzi za bibilia. Mawe haya yalitengenezwa kwa mfano wa bangili au mkufu. Zilivaliwa shingoni kuweza kufukuza maradhi, mashetani, na madhara na kuleta halinjema. Mungu aliwaonya wana waisraeli kuhusu manabii wauwongo na kuvaa mawe hayo ya kioo. Imeandikwa Ezekieli 13:18, 20, 21 "Useme Bwana mungu asema hivi; ole wao wanawake wale washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono wawekao leso juu ya vishwa vya kila kimo, ili wawinge roho za watu; je? Mtaziwinda roho zawatu watu wangu na kizihifadhi hai roho zenu wenyewe? Basi Bwana mungu asema hivi tazama mimi nikinyume cha hirizi zenu ambazo kwa hizo mna ziwinda roho za watu kama ndege nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu nami nitaziashilia roho zile mnazoziwinada kama ndege. Na leso zenu nitazirarua na kuwaokoa watu wangu katika mikono yenu wala hawatakuwa katika mikono yenu tena kuwindwa nanyimtajua yakuwa mimi ndimi Bwana."

Nivema kujua kuwa watu wengi wano husika na mawe au hirisi ni uchawi, Mungu anasema nini kuhusu ushawi? Imeandikwa Kumbukumbu la torati 18:9-12 "Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale. asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake katika moto, wala asionekane mtu atazamaye bao wala mtu atazamaye nyakati mbaya wala mwenye kubashiri wala msihiri, wala mtu alongaye kwa kupiga mafundo wala mtu apandizaye pepo wala mchawi wala mtu awaombao wafu, kwa kuwa mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana kasha ni kwasababu ya hayo Bwana, mungu wako amekufunza mbele yako."

Miujiza na ishara yawezakuwa kazi ya jule ibilisi au shetani imeandikwa 2Wathesalonike 2:9-10 "Yule ambaye kuja kwake nikwa mfano wa kutenda kwake shetani kwa uwezo wote na ishara na ajabu za uongo na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanao potea kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli wapate kuokolewa."

Uponyazi wa haki unatoka kwa mungu imeandikwa Zaburi 103:2-4 "Ee nafsi yangu umuhimidi Bwana wala usizisahau fadhili zake zote akusamehe maovu yako yote akuponya magojwa yako yote, aukomboa uhai wako na kaburi, akutia taji ya fadhili na rehema."

Wakati wa kiama wapiga hirisi hawata uridhi ufalme imeandikwa Ufunuo 22:14-15 "Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuwendea huo mti wa uzima na kuingia mjini kwa milango yake huko nje wako mbwa na wachawi na wazinzi na wauwaji nahao waabuduo sanamu na kila mtu apendaye uongo na kuufanya."