Kazi

Kazi yetu lazima tuifanye kwa heshima Imeandikwa Waefeso 6:7 "Kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu."

Mambo yote tunayoyafanya yawe ni ya kumtukuza Mungu Imeandikwa Wakolosai 3:17 "Nakila mfanyalo kwa neno au kwa tendo fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye."

Tufanye yote kwa moyo wote na wala si kwa udhaifu. Imeandikwa. Mhubiri 9:10 "Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya ulifanye kwa nguvu zako kwa kuwa hakuna kazi wala shauri wala maarifa wala hekima huko kuzimu uwendako wewe."