Kazi

Kazi zetu zote tuzifanye tukiwa na Kristo ndani yetu. Imeandikwa katika Wefeso 6:6-7 "Wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekezao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo."

Fanya kazi ukijua yakuwa Mungu ndiye atakayekagua kazi yako. Imeandikwa, 2Timotheo 2:15 "Jitahidi kujionyesha ya kuwa umekubaliwa na Mungu mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari ukitumia kwa halali neno la kweli."

Kuwa na ni fulani katika kazi ina umaana gani ua yaweza kusaidia? Imeandikwa Wakolosai 3:23 "Lo lote mfanyalo mfanyeni kwamoyo kama kwa Baba wala si kwa wanadamu." Mhubiri 9:10 yasema "Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya ulifanye kwa nguvu zako, kwa kuwa hakuna kazi wala shauri wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe."

Mtu ambaye hasaidii jamii yake ameikana imani. 1Timotheo 5:8 "Lakini mtu ye yote asiye watunza walio wake yaani wala wa nyumbani mwake hasa ameikana imani tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini."

Twaweza kupata somo jema katika maisha ya maumbile jinsi ya kufanya kazi. Imeandikwa katika Mithali 6:6-11 "Ewe mvivu mwendee chungu zitafakari njia zake ukapate hekima. kwa maana yeye hana akida wala msimamizi, wala mkuu, lakini hujiwekea akiba wakati wa jua hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. Ewe mvivu utalala hata lini? utaondoka lini katika usingizi wako? Bado kulala kidogo kusinzia kidogo Bado kukunja mikono upate usingizi Hivyo umaskini wako huja kama mnyang'anyi na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha."