Kiburi

Kuwa na kiburi ni hatari. Imeandikwa, Mithali 16:18 "Kiburi hutangulia uangamivu na roho yenye kutabakari hutangulia maanguko."

Kutakuwa na kiburi huleta heshima. Imeandikwa, Mithali 29:23. "Kiburi cha mtu kitamshusha bali mwenye roho ya unyeyekevu ataheshimiwa."

Mungu anashukia kiburi. Imeandikwa, 1 Petro 5:5-6 "Vivyo hivyo ninyi vijana watiini wazee naam ninyi nyote jifungeni unyenyekevu mpate kuhudumiana kwa sababu Mungu huwapiga wenye kiburi lakini huwapa wanyenyekevu neema basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu hilio hodari ili awakweze kwa wakati wake."

Kiburi shatutenga na Mungu na wenzetu. imeandikwa, Luka 18:14 "Nawaambia huyu alishuka kwenda kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana yule ajikwezaye atadhiliwa naye ajidhiliye atakwezwa."

Kuwa natabia kama ya mtoto mchanga ni ya muhimu mbinguni. Imeandikwa, Mathayo 18:4 "Basi ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni."

Wenye kiburi wataudhika. Imeandikwa, Mathayo 23:12 " Naye ye yote atakayejikweza atadhiliwa na ye yote atakayejidhili atakwezwa."

Wenye kiburi wataanguka. Imeandikwa, 1wakorintho 10:12 "Kwa hiyo anayejidhani kuwa amesimama aangaliye asianguke."