Kujaribiwa kwaweza kutuonyesha jinsi tulivyo. Imeandikwa, 2 Mambo ya nyakati 32:31 "Walakini kwa habari ya wajumbe wakuu wa babeli waliyotumwa kwake kuliza ajabu iliyofanywa katika nchi Mungu akamwacha ili amjaribu ili kwamba ayajue yote yaliyokuwamo moyoni mwake."
Kujaribiwa uweza kufanya tukuwe tukiezeshwa na Mungu. Imeandikwa, Zaburi 11:5 "Bwana humjaribu mwenye haki bali nafdi yake humchukia asiye haki na mwenye kupenda udhalimu."
Mungu anatuuliza tumjaribu kwa kutoa zaka zetu. Imeandikwa, Malaki 3:10 "Leteni zaka kamili ghalani ili kiweko chakula katika nyumba yangu mkanijaribu kwa njia hiyo asema Bwana wa majeshi mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka hata isiwepo nafasi ya kutosha au la."