Home / Masomo ya Biblia / Kusifika

Kusifika

Kusifika siyo siri ya furaha. Imeandikwa, Luka 6:26 "Ole ninyi watu wote watakapowasifu kwa kuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mabo kama hayo."

Shikilia imani yako hatakama hutasifika. Imeandikwa, Yohana 2:23-25 "Hata alipokuwa Yerusalemu kwenye sikukuu wakati wa pasaka watu wengi waliamini jina lake walipoziona ishara zake alizozifanya lakini Yesu hakujiaminisha kwao kwa kuwa yeye aliwajua wote na kwa maana sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu kwa maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo ndani ya mwanadamu."

Wale wanao funza neno la Mungu kwa kweli hawatasifika. Imeandikwa, 1Yohana 4:6 "Sisi twatokana na Mungu yeye amjuaye Mungu atusikia yeye asiyetokana na Mungu hatusikii katika hili twamjua Roho wa kweli na roho ya upotevu."