Home / Masomo ya Biblia / Kuzaliwa Upya Kiroho

Kuzaliwa Upya Kiroho

Kuweza kuingia katika ufalme wa Mungu lazima tuzaliwe upya katika kiroho. Imeandikwa, Yohana 3:3-8 "Yesu akajibu akawaambia, amini amini nawaambia, mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuuwona ufalme wa Mungu. nikodemo akamwambia awezaje mtu kuzaliwa akiwa mzee? aweza kuingia tumbini mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? Yesu akajibu amini, animi nakwambia mtu asipo zaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuiingia ufamle wa Mungu kilichozaliwakwa mwili ni mwili, kilichozaliwa kwa Roho ni roho usistaajabu kwa kuwa nilikwabia hamna budi kuzaliwa mara ya pili, upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia lakini hujui unakotoka wala unakokwenda kadhalika na hali yake kila mtu aliye zaliwa kwa Roho."

Uzima wa milele huanza wakati mtu anapozaliwa mara ya pili. Imeandikwa, Yohana 3:36 "Amwamiye mwana anauzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima wa milele bali ghadhabu ya Mungu inamkalia."

Kuzaliwa mara ya pili ina maana kufa kwa matendo ya mwili ya kale. Imeandikwa, Warumi 7:4 "Kadhalika ndungu zangu ninyi pia mmeifia torati kwa njia ya mwili wa Kristo mpate kuwa mali ya mwingine yeye aliyefufuka katika wafu kusudi tuzalie Mungu matunda."

Kuzaliwa tena huleta matokeo mapia mema na nia mpia. Imeandikwa, 1Yohana 3:9 "Kila mtu aliye zaliwa na Mungu hatendi dhambi kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu."