Mateso

Mateso hayaletwi kwa kutenda dhambi tu. Imeandikwa, Yohana 9:2-3 "Wanafunzi wake wakamwuliza waksema Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi hataazaliwe kipofu? Yesu akajibu akasema huyu hakutenda dhambi wala wazazi wake bali kazi za mungu zidhihirishwe ndani yake."

Yesu hakuahidi wanafunzi wake hawatapata mateso. Imeandikwa, Luka 21:17-19 "Nanyi mtachukuiwana watu wote kwa ajili ya jina langu walakini hautapote hata unywele mmoja wala vichwa vyenu nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu."

Yesu yupo pamoja nasi kwa wakati mgumu. Imeandikwa, Webrania 2:18 "Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa awezakuwasaidia wao wanaojaribiwa."

Twaweza kukuwa katika majaribu. Imeandikwa, Yakobo 1:2-3 "Ndugu zangu hesabuni yakuwa ni furaha tupu mkiangukia katika majaribu mbalimbali mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi."