Home / Masomo ya Biblia / Mpiga ramli

Mpiga ramli

Hali ya kupiga ramli imekatzwa na Mungu. Imeandikwa, Kumbukumbu la torati 18:9-13 "Utakapo kwisha ingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale asionekane mtu yeyote ampitishaye mwanawe au biti yake kati ya moto wala asionekane mtu atazamaye bao wala mtu atazamaye nyakati mbaya wala mwenye kubashiri wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo wala mtu apandishaye pepo wala mchawi wala mtu aombaye wafu kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kasha ni kwa sababu ya hayo Bw ana Mungu wako, anawafukuza mbele yako."

Mungu ndiye ajuaye mambo yajayo. Imeandikwa, Isaya 8:19 "Nawakati watakapokuambia tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi walio na ndege na kunong, ona je! haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je waende kwa watu walio kufa kwa ajili ya watu walio hai?."