Home / Masomo ya Biblia / Mtindo wa Maisha

Mtindo wa Maisha

Lazima tuwe na nidhamu katika maisha yetu. Imeandikwa 1Wakorintho 9:24-25 "Je! hamjui ya kuwa wale washindanao kwa kupinga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja, pigeni mbio namna hio ilimpate. Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote basi hao hufanya hivyo kusudi wapate taji iharibikayo bali sisi tupate taji isiyoharibika."

Maisha yetu lazima yawesambamba na neno la Mungu. Imeandikwa, 2Timotheo 2:15 "Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu mtenda kazi asiye sababu ya kutahayari ukutumia kwa halali neno la kweli."