Ngono

Hali ya kuonana kimwili ni zawadi kutoka kwa Mungu inapofanywa katika ndoa kwa raha zao. Imeandikwa, Mithali 5:18-19 "Chemchemi yako ibarikiwe nawe umfurahiye mke wa ujana wako ni ayala apendaye na paa apendezaye maziwa yake yakutoshe sikuzote na kwa upendo wake ushangilie daima."

Kufuraiana na kuonana kimwili ni jambo la kutiliwa maanani katika ndoa. Imeandikwa, Waebrania 13:4 "Ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi kwamaana washerati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu." 1Wakorintho 7:3, 4 Yasema "Mume ape mke wake haki yake na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake mke hana amri juu ya mwili wake bali mumewe vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake bali mkewe."

Mungu aliumba hali ya kuonana kimwili kuwa uhusiano katika ya mke na mume katika ndoa. Imeandikwa, 1Wakorintho 7:5 "Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda ili mpate faragha kwa kusali mkajiane tena shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu."

Tusije tukajikwaa nivema tuweke mahitaji ya. zinaa katika uwezo wa Mungu. Imeandikwa, 1Wathesalonike 4:3-5 "Maana haya ndiyo mapezi ya Mungu kutakazwa kwenu muepukane na uasherati kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima si katika hyali ya tamaa mabaya kama mataifa wasiomjua Mungu."

Amri ya saba ya onnya kuzini. Imeandikwa, Kutoka 20:14 "Usizini".

Zinaa ni kubaya ikifanywa nje ya ndoa, ijapokuwa hatuwezi kuona matokeo yake hapo kwa hapo. Ieandikwa, 1wakorintho 6:18 "Ikimbie zinaa kila dhambi aitendayo mwanadamu ni aya nje ya mwili wake ila afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe."

Dhambi ya zinaa ya anzaa vipi?. Imeandikwa, Mathayo 5:28 "Lakini mimi nawaambia kila mtu atazamaye mwanake kwa kutamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake."

Bibilia ya onya zinaa kati ya mwanamume na mwanamume au mwanamke na mwanmke. Imeandikwa, Warumi 1:26-27 "Hivyo Mungu aliwaasha wafuate tama zao zaa aibu hataa wanawake wakabadili matumizi yasiyo ya asili wanaume nao vivyo hivyo waliasha matumizi ya mke ya asili wakawakiana tamaa wanaue wakiyatenda yasiyo wapasa wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao."

Bibilia yaonya zinaa kati ya ndugu na dada. Imeandikwa, Mambo ya walawi 18:6 "Mtu ye yote aliye wakwenu asimkaribie mweziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua atupu mimi ndimi Bwana."

Bibilia yaonya zinaa na wanyama. Imeandikwa, Mambo ya walawi 18:23 "Wala usilale na mnyama ye yote ili kujitia unajisi kwake wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye ni uchafuko."

Bibilia ya onya kufanya mapenzi na kahaba. Imeandikwa, 1Wakorintho 6:15-17 "Je hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? na kuvifanya viungo vya kahaba? hasha au hamjui yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili moja naye lakini yeye aliye ungwa na Bwana ni roho moja naye."