Ubaguzi

Sote tu kitukimoja katika kritsto. Imeandikwa, Wagalatia 3:28 "hapana myahudi wala myunani hapana mtumwa wala huru hapana mtu mume wala mtu mke maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika kristo Yesu."

Chuki baina ya jamaa ya rangi au kabila ni dhambi. Imeandikwa, Yakobo 2:8-9 "Lakini mkitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa mpendeni jirani yako kama nafsi yako mwatenda vema. Bali mkiwapendelea watu mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sheria kuwa wakosaji."

Sote tuna damu sawa. Imeandikwa, Matendo ya mitume 17:26 "Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja wakae juu ya uso wa nchi jote akisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu awali na mipaka ya kazi yao."

Mungu anakubali watu wakila taifa na jamaa na lugha. Imeandikwa, Matendo ya mitume 10:34-35. "Petro akafumbua kinywa chake hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye."