Uchawi

Mungu ametuonya dhidi ya uchawi. Imeandikwa, Kumbukumbu la torati 18:9-13. "Utakapo kusha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake katika motowala asionekane mtu atazamaye bao wala mtu atazamaye nyakati mbaya wala mwenye kubashiri wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo wala apandishaye pepo wala mchawi wala mtu awaombaye wafu." kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana kasha ni kwa sababu ya hayo Bwana Mungu wako anawafukuza mbele yako. Uwe mkamilifu kwa Bwana Mungu wako."

Wanao fanya uchawi hawatauridhi ufalme wa Mungu. Imeandikwa. Wagalatia 5:19-21 "Basi matendo ya mwili ni dhahiri ndiyo haya uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu uchawi, uadui, ugomvi, wivi hasira fitina, faraka uzushi, husada, ulevi, ulafi na mambo yanayofanana na hayo. Katika hayo na waambia mapema kama nilivyokwisha kuwaambia watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawatauridhi ufalme wa Mungu."

Hakuna mtu ajuaye sutakavyo kuwa sikuzijazo. Imeandikwa, Isaiya 8:19, "Na wakati watakapokuambia tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi waliao kama ndege na kunong'gona; Je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao, Je! Waende kutafuta habari kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai."