Uvivu

Uvivu mwingi usiruhusiwe. Imeandikwa, 2Wathesalonike 3:11-12 "Maana twasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu hawana shuguli zao wenyewe lakini wanajishugulisha na mamba ya wengine basi twaagiza hao na kuwaonya katika Bwana Yesu kristo watende kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe."

Kufanya kazi kwa bidii kwaonyesha tabia njema ya mkristo. Imeandikwa, 2Timotheo 2:15 "Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari ukitunmia kwa halali neno la kweli."

Watu wavivu hawawezi kufanikiwa. Imeandikwa, Mithali 10:4-5 "Atendaye kazi kwa mkono mlegevu huwa maskini bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima bali asinziyaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha."

Watu wavivu hawana uamuzi mwema. Imeandikwa, Mithali 26:13-16 "mtu mvivu husema simba yuko njiani simba yuko katika njia kuu kama vile mlango ugeukavyo katika bawaba zake kadhalika mtu mvivu katika kitanda chake mtu mvivu hutia mkono wake sahanini kwa mchosha kuupeleka kinywani pake Mtu mvivu nimwenye hekima machoni pake kuliko watu saba wawezao kutoa sababu."

Kuna somo kutokana na wadudu. Imeandikwa, Mithali 6:6-11 "Ewe mvivu mwendee chungu zitafakari njia zake upate hekima kwa maana yeye hana akida wala msimamizi wala mkuu lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua hukusanya chakula chake wakati wa mavuno ewe mvivu utalala hata lini? utondokalini katika usingizi wako bado kulala kidogo kusinzia kidogo bado kukuja kono upate usingizi hivyo umaskini wako huja kama mnyanga'anyi na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha."