Twpata uwezo wa Mungu kupitia kwa Roho mtakatifu. Imeandikwa, Matendo ya mitume 1:8 "Lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho mtakatifu nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu na katika Uyahudi wote na Samaria na hata mwisho wa nchi."
Mungu anauwezo wa kuumba. Imeandikwa, Mwanzo 1:1 "Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi."
Mungu anauwezo juu ya nguvu za ulimwengu. Imeandikwa, Marko 4:39-41 "Akaamka akaukemea upepo, akaiambia bahari nyamaza utulie. upepo ukakoma kukawa shwari kuu, akawaambia mbona mmekuwa waoga? hamna imani bado? wakaingiwana hofu kuu wakaambiana ni nani huyu basi hata upepo na bahari kumtii?.
Yesu anauwezo juu ya magonywa na maradhi. Imeandikwa, Mathayo 4:23 "Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote na kuihubiri habari njema ya ufalme na kuponya ugonywa na udhaifu wa kila namna katika watu."
Mungu anauwezo juu ya mashetani. Imeandikwa, Marko 6:7 "Akawaita wale thenashara akaanza kuwatuma wawili wawili akawapa amri juu ya pepo wachafu."
Mungu anauwezo juu ya kifo. Imeandikwa, Ufunuo 21:4 "Naye atafuta kila chozi katika macho yao wala mauti haitakuwapo tena wala maombolezo wala kilio wala maumivu hayatakuwapo tena kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita."
Mungu ametupa uwezo wakuwa wanawake. Imeandikwa, Yohana 1:12 "Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wakufanyika watoto wa Mungu ndio wale waliaminio jina lake."
Maombi ya mwenye haki ina nguvu na hutimilika. Imeandikwa, Yakobo 5:16 "Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana mpate kuponywa kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii."
Hasira hupa shetani hafasi katika moyo wako. Imeandikwa, Waefeso 4:27 "Msimpe Ibilisi na fasi."
Kujipa kwako kwa Mungu hukupa nguvu zakuyashinda majaribu. Imeandikwa, Yakobo 4:7 "Basi mtiini Mungu, mpingeni shetani naye atawakimbia."
Naweza kuwa na uwezo wa Yesu niweze kuishi maisha ya kikristo. Imeandikwa, Wafilipi 4:13 "Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu."
Neno la Mungu lina uwezo mkuu. Imeandikwa, Waebrania 4:12 "Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu tena lina ukali kuliko uwao wote ukatao kuwili tela lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake, tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo."