Home / Masomo ya Biblia / Vipaji vya Roho

Vipaji vya Roho

Ingawaje vipaji vyetu vya Roho havifanani vyote vina tumika kumtumikia Mungu. Imeandikwa, Warumi 12:4-5 "Kwa kuwa kama vile mwili mmoja kuna viungo vingi wala viungo vyote havitendi kazi moja; vivyo hivyo nasi tulio wengi tu mwili mmoja katika Yesu Kristo, na viungo kila mmoja kwa mwenzake."

Vipaji vya Roho vyatoka kwa Mungu kwa kazi yake. Imeandikwa, 1Wakorintho 12:4-6 "Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule, kasha pana tofauti za kutenda kazi bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote."

Je! Vipaji vya Roho Ni vipi? Imeandikwa, 1Wakorintho 12:8-11 "Maana mtu oja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine la maarifa apendavyo Roho yeye yule, mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii, na mwingine kupambabua roho, mwingine aina za lugha lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye." Waefeso 4:11-13 yasema hivi "Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu kwa kusudi kuwakamilisha watakatifu hata kazi ya huduma itendeke hata mwili wa Kristo ujengwe. Hata na sisi tutakapo ufikia umoja wa iani na kumfahamu sana mwana wa Mungu hata kuwa mtu mkamilifu hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo."