Home / Masomo ya Biblia / Wachungaji

Wachungaji

Askofu lazima awe mwaminifu kwa jamii yake na anayefanya kulingana na Mungu. Imeandikwa, 1Timotheo 3:2- 7 " Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika mme na mke mmoja mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha, si mtu wakuzoea ulevi, si mpiga watu bali awe mpole si mtu wa kujadiliana wala asiwe mwenye kupenda fedha mwenye kuisimamia nyumba yake vema ajuaye kutiisha watoto wake katika ustahivu yani mtu asiye jua kuisimamia nyumba yake mwenyewe atalitunzaje kanisa la Mungu? Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya ibilisi tena amempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje iliasianguke katika lawama na mtego wa ibilisi."

Askofu asiwe wa kutafuta madaraka. Imeandikwa, 1Wakorintho 4:6 "Basi ndugu mambo hayo nimeyafanya kwa mfano wa mimi na Apolo kwa jili yenu ilikwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupata yale yaleyaliyoandikwa ilimmoja wenu asijivune kwa jili ya huyu kinyume cha mwenziwe."

Askofu lazima wawafunze watu neno la Mungu kwa kutumia neno la Mungu na kufanya lizavosema. Imeandikwa, Matendo ya mitume 20:28 " Jitunzeni nafsi zenu na lile kundi lote nalo ambalo Roho mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake mpate kulilisha kanisa lake Mungu alilolinunua kwa damu yake mwenyewe."