Home / Masomo ya Biblia / Walimwengu

Walimwengu

Ukimpenda Mungu mambo ya dunia hayatakuwa tena na mvuto. Imeandikwa katika 1Yohana 2:15-17 "Msiipende dunia na mambo yaliyomo katika dunia, mtu akiipenda dunia kumpenda Baba hakumo ndani yake maana kila kilichomo duniani yaani tamaa ya mwili, na taama ya macho na kiburi cha uzima havitokani na Baba bali vyatokana na dunia na dunia inapita pamoja na tamaa zake bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele."

Huwezi kufurahia anasa za ulimwengu na kuwa rafiki wa Mungu. Imeandikwa katika Yakobo 4:4 "Enyi wazinzi hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakayekuwa rafiki wa dunia ajifanya kuwa adui wa Mungu."

Je! Ni mambo gani ambayo ni mabaya? Imeandikwa katika Wagalatia 5:19-21 "Basi matendo ya mwili ni dhahiri ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo katika hayo nawaambia mapema kama nilivyokwisha kuwaambia watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu."

Usifuate mambo yanayopendwa na dunia yasiyo mema. Imeandikwa katika Warumi 12:2 "Wala msifuatishe namna ya dunia hii bali geuzwe kwa kufanywa upya nia zenu pate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema ya kumpendeza na ukailifu."

Kumjua Yesu kunakata tamaa za ulimwengu. Imeandikwa katika Wagalatia 6:14 "Lakini mimi hasha nisione fahari ya kitu cho chote, ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambao kwa huo ulimwengu umesulubishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu."

Epukana na elimu za walimwengu. Imeandikwa katika Wakolosai 2:8 "Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu ya bure na madanganyo matupu kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu wala si kwa jinsi ya Kristo."

Ishi kama makao yako, yako mbinguni. Imeandikwa, 1 Petro 2:11 "wapenzi na wasi hi kama wapitaji na wasafiri ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na Roho."