Home / Masomo ya Biblia / Watoto wa Mungu

Watoto wa Mungu

Ninani mwana wa Mungu? kuzaliwa kwa kiroho hufanya mtu kuwa mwana wa Mungu. Imeandikwa Yohana 1:12-13 "bali waliompokea aliwapa uwezo wakufanyika watoto wa Mungu ndio wale waliaminio jina lake walio zaliwa sikwa damu wala si kwa mapenzi ya mwili wala sikwa mapenzi ya mtu bali kwa Mungu."

Mungu amefungua njia yakuwa watoto wake. Imeandikwa 1Yahana 3:1 "Tazameni ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu na ndivyo tulivyo kwa sababu hii ulimwengu haututambui kwa kuwa aukutambua yeye."

Wakristo wamefanywa kuwa jamaa ya Mungu imeandikwa Warumi 8:16 "Roho mwenywe hushuudia pamoja na roho zetu ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu."

Tazama watoto washanga. imeandikwa Luka 18:16-17 "Bali Yesu akawaita waje kwake, akasema waasheni watoto wadogo waje kwangu wala msiwazuie kwa kuwa watu kama hao ufalme wa Mungu ni wao amininawaambia, mtu yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hauingii kamwe."