Wazee

Ni lazima tuwape watu wazee heshima. Imeandikwa, Mambo ya walawi 19:32 "Mwondokeeni mtu mwenye mvi heshimuni uso wa mtu mzee nawe mche Mungu wako, mimi ndimi Bwana."

Wazee waume kwa wake lazima tuwape heshima. imeandikwa, 1Timotheo 5:1 "Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba na vijana kama ndugu." na wanawake wazee kama mama wana wake vijana kama ndungu wa kike katika usafi wote."

Watu wazee na wapewe umanaa kama watu wenye ujuzi na ufahamu. Imeandikwa Mithali 20:29 "Fahari ya vijana ni nguvu zao na uzuri wa wazee ni kichwa chenye mvi."

Vijana waweza kuelimika katika maicha yao kutokana na maisha ya wazee. Imeandikwa, Zaburi 71:18, "Na hatanikiwa mzee mwenye mvi, Ee Mungu usiniache. hata niwaeleze watu wakizazi hiki nguvu zako na kila atakayekuja uwezo wako."

Kuna mawaidha kwa watu wazee. Imeandikwa, Tito 2:2-5 "Ya kwamba wazee wawe wenye kiasi, wastahivu, wenye busara wazima katika imani na wenye upendo na katika saburi vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu wasiwe wasingiziaji wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi bali wafundishao mema ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao na kuwapenda watoto wao na kuwa wenye kiasi kuwa safi kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema kuwatii waume zao wenyewe ili neno la Mungu lisitukanwe."