Amani

Naweza kupata amani vipi? Imeandikwa Ayubu 22:21 "Mjue sana Mungu ili mwena amani ndivyo mema yatakavyokujia."

Amani nikufanya mambo yako kuwa sawa na Mungu au kuwana uhusiano mwema na Mungu. Imeandikwa, Warumi 5:1 "Basi tukisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani na mwe na amani kwa Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu kristo."

Amani ni zawadi kutoka kwa Mungu. Imeandikwa, Yohana 14:27 "Imani na waachieni, amani yangu na wapa niwapovyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo msifadhaike mioyoni mwenu wala msiwe na woga."

Amani huja kwa njia ya kuzitii amri za Mungu. Imeandikwa, Zaburi 119:165 "Wana amani nyingi waipendao sheria yako wala hawna la kuwakwaza."

Nivema kuwa na nia ya kutafuta amani. Imeandikwa, Warumi 14:19. "Basi kama ni hivyo na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana."

Amani ni ngao. Imeandikwa, Zaburi 122:6-7 "Utakieni Yerusalemu amani na wafanikiwe wakupendao amani na ikaendani ya kuta zako."

Je nawezaje kuiweka amani ambayo nimeipata?. Imeandikwa, Isaya 26:3-4 "Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea katika amani kamilifu kwa kuwa anakutumaini mtumaini Bwana siku zote maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele."

Furaha huja kwa kuw na mapatano mema na watu. Imeandikwa, Mathayo 5:9 "Heri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu."