Home / Masomo ya Biblia / Burudani

Burudani

Kuna mambo muhimu unapo changua raha au anasa pamoja na vitabu, miziki, televisheni au senema imeandikwaWafilipi 4:8 "Hatimaye ndugu zangu mambo yo yoye yalio ya kweli, yo yote yalio ya staha yo yote yalio ya haki yo yote yalio safi yo yote yenyekupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote ikiwapo sifa nzuri yo yote yatafakarini hayo."

Jitenge na mambo yasiyo mema imeandikwa Zaburi 101:3 "Sitaweka mbele ya macho neno la uovu kazi ya walio potoka naichukia haitaambatana nami."

Hauwezi kufurahia anasa nyingi zaulimwengu na uwe rafiki wa mungu imeandikwa Yakobo 4:4 "Enyi wazinzi hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia nikuwa adui wa mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa mungu."

Ni ansa gani mbaya za ulimwengu? Imeandikwa Wagalatia 5:19-21 "Basi matendo ya mwili ni dhahiri ndiyo haya, uasherati uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi husuda, ulevi, ulafi na mambo yanayofafanana na hayo katika hayo nawambia mapema kama nilivyokwisha kuwaambia ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawatauridhi ufalme wa mungu."

Pia Imeandikwa 1Yohana 2:15-17 "Msipende dunia wala mambo yaliyomo katika dunia mtu akipenda dunia kumpenda baba hakumo ndani yake maana kila kilichomo duniani yani tamaa ya mwili, na tamaa ya macho na kiburi cha uzima havitokani na Baba balivyatokana na dunia na dunia inapita pamoja na tamaa zake bali yeye afanyaye mapenzi ya mungu adumu hata milele."

Mambo yote tunayo yafanya yapaswa kuamabtana na jina la mungu imeandikwa Wakolosai 3:17 "Nakila mfanyalo kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru mungu Baba kwa yeye."