Dhamana

Mungu ametuweka katika hali ya thamani kuu katika Uumbaji wake. Imeandikwa, Zaburi 8:3-5 "Nikiziangalia mbingu zako kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha. Mtu ni kitu gani hata umkumbuke na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu umemvika taji ya utukufu na heshima."

Mungu anatuthamini hawezi kututoa katika mawazo yake. Imeandikwa, Zaburi 139:17-18 "Mungu fikira zako zina thamani nyingi kwangu jinsi ilivyo kubwa jumla yake kama ningezihesabu ni nyingi kuliko mchanga. Niamkapo nikali pamoja nawe."

Jambo la muhimu katika maisha yetu nikuwa na uraia wa mbinguni. Imeandikwa, Mathayo 13:44. "Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyo sitirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona aliificha na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile."

Jambo la muhimu ni kudhamini maisha yako na kufikiri juu ya ufalme wa Mungu. Imeandikwa, Mathayo 16:26 "Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata uliwengu wote na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?". Wakolosai 3:2 yasema "Yafikirini yaliyo juu sio yaliyo katika nchi."